Jumatano 11 Juni 2025 - 20:18
Uigizaji wa Tukio la Ghadir kufanyika katika maeneo 149 nchini Iran

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Khudadode ametangaza kuhusiana na mipango mbalimbali ya kiutamaduni, kijamii na mchakato mzima wa siku kumi za Wilaya za Sikukuu ya Ghadir, huku akisisitiza kuwa mwaka huu kipindi hicho kitaadhimishwa kwa msisitizo maalum juu ya "Nahjul Balagha", kuimarisha maudhui ya sherehe, kampeni ya kuwaachilia wafungwa, utoaji wa chakula kwa umma kwa wingi, pamoja na kuigiza upya tukio la kihistoria la Ghadir katika maeneo 149 ya nchi nzima.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Kamal Khudadode, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Uratibu la Shirika la Tablighi la Kiislamu, katika kikao kilichoandaliwa kwa heshima ya maadhimisho ya siku kumi za Uimamu na Wilaya pamoja na Sikukuu adhimu ya Ghadir, alieleza kwamba: siku kumza Uimamu na Wilaya ni fursa muhimu kwa taasisi zote za tablighi nchini kutumia uwezo wao wa kimatendo na wa kimapokezi kwa ajili ya mada hii nyeti.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha